Mhubiri Mlango 11 Ecclesiastes

Mhubiri 11:1 Ecclesiastes 11:1

Tupa chakula chako usoni pa maji; Maana utakiona baada ya siku nyingi.

Mhubiri 11:2 Ecclesiastes 11:2

Uwagawie sehemu watu saba, hata wanane; Maana hujui baa gani litakalokuwa juu ya nchi.

Mhubiri 11:3 Ecclesiastes 11:3

Mawingu yakiwa yamejaa mvua, Yataimimina juu ya nchi; Na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini, Paangukapo ule mti, papo hapo utalala.

Mhubiri 11:4 Ecclesiastes 11:4

Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.

Mhubiri 11:5 Ecclesiastes 11:5

Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.

Mhubiri 11:6 Ecclesiastes 11:6

Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiuzuie mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa,kama ni hii au hii,au kama zote zitafaa sawasawa.

Mhubiri 11:7 Ecclesiastes 11:7

Kweli nuru ni tamu, tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua.

Mhubiri 11:8 Ecclesiastes 11:8

Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili.

Mhubiri 11:9 Ecclesiastes 11:9

Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.

Mhubiri 11:10 Ecclesiastes 11:10

Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.